Luke 20:1-8

Swali Kuhusu Mamlaka Ya Yesu

(Mathayo 21:23-27; Marko 11:27-33)

1 a bSiku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wa watu wakamjia. 2 cWakamuuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

3Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. 4 dJe, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”

5Wakahojiana wao kwa wao wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 6 eLakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii.”

7Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.”

8Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Copyright information for SwhNEN